Loading...

Jezi mpya ya Arsenal itakayotumika msimu wa 2017/18


Arsenal imeonyesha uzi wao wa nyumbani katika msimu wa 2017/18. Hata hivyo uzi huo hautofautiani sana na ule wa msimu uliomalizika.

Jezi hizo zimetolewa mapema na wadhamini Kampuni ya Puma ili watu waanze kuzoea na kununua kabla ya kuanza kwa msimu.

Uzi huo utavaliwa kwa mara ya kwanza na kikosi cha Arsenal wakati watakapopambana kwenye mechi ya kuwania ngao ya hisani.

Watavaa kwa mara ya pili katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Leicester Uwanjani Emirates, Agosti.
Jezi mpya ya Arsenal itakayotumika msimu wa 2017/18 Jezi mpya ya Arsenal itakayotumika msimu wa 2017/18 Reviewed by Zero Degree on 6/21/2017 08:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.