Loading...

Kwa uamuzi huu, ..inaweza kuwa ahueni kwa Chelsea na mbaya kwa Manchester United

Antonie Griezmann, Atletico Madrid
Chelsea, Manchester United, Lyon na klabu nyingine bora Ulaya zimeathiriwa kwa uamuzi uliochukuliwa asubuhi ya leo nchini Switzerland.

Uamuzi huo umefanya mambo kuwa magumu katika soko la usajili katika majira ya joto pamoja na klabu nyingi na wachezaji wengi kuhusika. Mahakama imelizingatia suala la klabu ya Atletico Madrid kufungiwa kufanya usajili, ikiwa inamaana kwamba hawataweza kununua mchezaji yeyote hadi mwezi January 2018.

Hiyo inamaana kwamba, kama Atletico hawaruhusiwi kununua mchezaji yeyote katika majira ya joto, ni dhahiri kwamba hawatauza mchezaji yeyote aidha. Hapo moja kwa moja unamfikiria mchezaji mmoja, Antonie Griezmann! Man United hakika watakuwa wameshaanza kutafuta mbadal mwingine baada ya kugundua kwamba, nguvu na juhudi zote walizofanya hazijazaa matunda yoyote. 
Diego Costa, Chelsea
Mchezaji mwingine aliyeathiriwa na uamuzi huo ni wa Chelsea, Diego Costa hakika! Inaonekana kwamba Costa ataendelea kubakia Chelsea.

Diego Costa hivi karibuni amejitokeza na kukanusha taarifa zote zilizokuwa zikimuhusisha na uhamisho kuelekea Klabu inayoshiriki Ligi kuu ya China. Zote zilikuwa ni habari za uongo zilizotolewa na baadhi ya mitandao na television. Hata hivyo, Costa pia alisema kuwa aengeondoka Chelsea endapo tu ingekuwa ni kwa kurejea katika klabu yake anayoipenda, Atletico Madrid. Hilo tayari suala ambalo liko juu ya uwezo wake. Chelsea imefanikiwa kushinda vita ya kwanza katika usajili wa wachezaji msimu huu wa majira ya joto!

Alexandre Lacazette, Lyon
Uamuzi huo pia umetibua dili la Atletico, ambao walikuwa wanamsaka nyota wa Lyon, Alexandre Lacazette. Lyon wanaweza kulazimika kumuuza nyota wao kwa klabu nyingine kubwa yoyote ya Ulaya kwa sasa ambapo Lacazette bila shaka atakuwa anahitaji kulionja joto la Ligi ya Mabingwa wakati Lyon wanauwezo wa kuishia Ligi ya Europa.

Usishangae kusikia Chelsea, Manchester United na Manchester City wataingia vitani kumsaka Lacazette ijapokuwa Arsenal wanaweza kuwa wakwanza kwa kupeleka ofa ya pauni milioni 10 lakini sio lazima wafanikiwe kumnyakua nyota huyo kwani anaweza kugeuka lulu.

Adhabu hiyo ya Atletico kufungiwa kusajili ilitokana na kusajili wachezaji wa nje wenye umri chini ya miaka 18. Real Madrid pia walikumbwa na adhabu hiyo lakini baada ya kukata rufaa walifanikiwa kupunguziwa adhabu. Hiyo itaibua mlolongo wa malalamiko ya kudai haki haitendeki ambao Atletico, Barcelona na klabu nyinginezo zimekuwa zikilalamikia na unaweza kuona ni kwanini!
Kwa uamuzi huu, ..inaweza kuwa ahueni kwa Chelsea na mbaya kwa Manchester United Kwa uamuzi huu, ..inaweza kuwa ahueni kwa Chelsea na mbaya kwa Manchester United Reviewed by Zero Degree on 6/01/2017 07:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.