Loading...

Lowassa ahojiwa na polisi kwa saa nne na kuachiwa kwa dhamana


Aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh. Edward Lowassa amehojiwa na polisi kwa muda wa saa nne na baade kuachiwa baada ya kujidhamini mwenyewe huku ulinzi ukiimarishwa kuzunguka makao makuu ya jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuachiwa Mh.Lowassa mbali na kueleza kwa ufupi sababu za kuhojiwa amesema anatakiwa kurudi tena polisi siku ya Alhamisi saa sita mchana.

Mwanasheria wake Bw.Peter Kibatala ambaye alikuwa ameongozana naye amesema hatima ya alichoitiwa itajulikana Alhamisi kama wataenda Mahakamani au la huku katibu mkuu wa Chadema Dkt. Vicent Mashinji akizungumzia msimamo wa chama chake juu ya suala hilo.

Hata hivyo majira ya asubuhi waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari walifika kituo kikuu cha polisi ili kupata taarifa kuhusiana na tukio hilo bila mafanikio baada ya kuzuiliwa kungia na kutakiwa kuondoka maeneo, na ulinzi ukiwa umeimarishwa likiwemo gari la maji ya kuwasha.
Lowassa ahojiwa na polisi kwa saa nne na kuachiwa kwa dhamana Lowassa ahojiwa na polisi kwa saa nne na kuachiwa kwa dhamana Reviewed by Zero Degree on 6/28/2017 11:49:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.