Mama adanganywa kwa kupewa shilingi elfu 10 kisha aibiwa mtoto wa miezi 4 jijini Mwanza
Imeelezwa kuwa watu waliomuiba mtoto huyo wamemchukua mama mzazi wa motto huyo kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani lakini baada ya kufika Nyamanoro walimpa shilingi elfu kumi kwenda kununua mkate na baada ya kurudi amekuta tayari wameshaondoka na mtoto wake.
Wakizungumzia kuhusu tukio hilo baadhi ya wananchi wamesema kuwa jambo hilo limewashangaza kwani wameshindwa kuelewa lengo la watu hao kumuiba mtoto huyo ni nini na kuwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa watu waliofanya tukio hilo mama mzazi wa mtoto anawafahamu hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu hao.
Hata hivyo Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuwasaka watu waliohusika na kumuiba mtoto huyo na kwamba watakapobainika watafikishwa katika vyombo vya dola.
Wakizungumzia kuhusu tukio hilo baadhi ya wananchi wamesema kuwa jambo hilo limewashangaza kwani wameshindwa kuelewa lengo la watu hao kumuiba mtoto huyo ni nini na kuwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa watu waliofanya tukio hilo mama mzazi wa mtoto anawafahamu hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu hao.
Hata hivyo Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuwasaka watu waliohusika na kumuiba mtoto huyo na kwamba watakapobainika watafikishwa katika vyombo vya dola.
Mama adanganywa kwa kupewa shilingi elfu 10 kisha aibiwa mtoto wa miezi 4 jijini Mwanza
Reviewed by Zero Degree
on
6/29/2017 10:31:00 AM
Rating: