Loading...

Watu 63 wamekamatwa na Tanesco wilayani Manyoni kwa wizi wa umeme


Shirika la umeme Tanzania Tawi la Singida limewakamata watu sitini na tatu katika kijiji cha Mitundu halmashuri ya Itigi wilayani Manyoni, ambao wanaliibia shirika kwa kujiunganishia umeme kwa njia ya kukwepesha kupitia katika mita na wengine kutokuwa na mita na kulisababishia shirika kupata hasara.

Afisa usalama wa TANESCO mkoa wa Singida Bwana Juma Mahuba amesema kutokana na kupata taarifa kwa wasamaria wema,wamefanikiwa kuwa kamata watu hao,ambao walikuwa wakiiba umeme kwa kukwepesha katika mita na kujiunganishia moja kwam oja.

Akithibitisha kuibiwa kwa umeme huo Mwenyekiti wa kijiji cha Mitundu Bwana Andrea Mlewa,amesema chanzo kikubwa ni kucheleweshwewa kuunganishiwa umeme,na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO Itigi kuaua kuwaunganishia umeme watu kwa kutoa fedha,huku walio unganishiwa umeme wakimtaja mfanya kazi huyo.

Operesheni hiyo ambayo imefanyika katika kijiji cha Mitundu halmashauri ya Itigi pamoja na kuwakamata watu hao ,wata hakikisha wanafikishwa mahakamani wakiweo baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO kwa kuwa unganishia umeme kinyume na taratibu za TANESCO.
Watu 63 wamekamatwa na Tanesco wilayani Manyoni kwa wizi wa umeme Watu 63 wamekamatwa na Tanesco wilayani Manyoni kwa wizi wa umeme Reviewed by Zero Degree on 6/29/2017 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.