Mbaraka Yusuph azitosa Simba na Yanga
Mbaraka ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa msimu 2016/17 anatajwa pia kuwindwa na klabu za Simba na Yanga zote za jijini.
Taarifa zilizopatikana jijini jana zinasema kuwa Mbaraka anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili baada ya kuridhika na ofa ambayo Azam FC imeahidi kumpatia chipukizi huyo ambaye aliichezea Simba kabla ya kwenda Kagera Sugar.
Akizungumza na Gazeti la Nipashe jana, Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa 'Father', alisema kuwa ni kweli klabu yake imefanya mazungumzo na mshambuliaji huyo yamefikia hatua nzuri.
Idrissa alisema kuwa wanatarajia ujio wa mshambuliaji huyo utaongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Msimu uliopita Mbaraka alifunga mabao 13 huku Simon Msuva wa Yanga na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting walioshinda tuzo ya kiatu cha dhahabu wakifunga mabao 14 kila mmoja.
Kutokana na kuonyesha kiwango cha juu, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga alimuita mshambuliaji huyo katika kikosi chake na akicheza kwa mara ya kwanza alifunga bao la ushindi wakati timu hiyo ilipoifunga Burundi mabao 2-0.
Tayari Azam inayonolewa na kocha Aristica Cioaba kutoka Romania imeshamsajili mshambuliaji wa Toto Africans ya jijini Mwanza, Waziri Junior.

"Ni kweli tumefanya mazungumzo na Mbaraka, ni mchezaji ambaye yuko katika mipango yetu, tunasubiri kwanza amalize jukumu la taifa," alisema kwa kifupi katibu huyo.
Msimu uliopita Mbaraka alifunga mabao 13 huku Simon Msuva wa Yanga na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting walioshinda tuzo ya kiatu cha dhahabu wakifunga mabao 14 kila mmoja.
Kutokana na kuonyesha kiwango cha juu, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga alimuita mshambuliaji huyo katika kikosi chake na akicheza kwa mara ya kwanza alifunga bao la ushindi wakati timu hiyo ilipoifunga Burundi mabao 2-0.
Tayari Azam inayonolewa na kocha Aristica Cioaba kutoka Romania imeshamsajili mshambuliaji wa Toto Africans ya jijini Mwanza, Waziri Junior.
Credits: Nipashe
Mbaraka Yusuph azitosa Simba na Yanga
Reviewed by Zero Degree
on
6/10/2017 10:03:00 AM
Rating: