Loading...

Michuano ya SportPesa Super Cup itaendelea tena kesho


Hii leo ni mapumziko ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kushuhudia timu kadhaa kutinga hatua ya nusu fainali huku baadhi zikiyaaga mashindano hayo makubwa na yenye mvuto wa kipekee.

Mashindano hayo yalioanza kutimua vumbi rasmi siku ya jumatatu ya tarehe 5 ya wiki hii , wadau wa soka wameshuhudia timu za Tanzania zikishindwa kufanya vyema katika michuano hiyo.

Miongoni mwa timu zilizoyaaga mashindano haya mapema tu ni klabu ya Singida United, Jang’ombe Boys kutoka Zanzibar, Tusker ya Kenya pamoja na Simba SC ya Tanzania.

Klabu zilizopata nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup ni Dar young Africans, Gor Mahia ya nchini Kenya, AFC Leopard ‘Ingwe’ pamoja na Nakuru All Stars zote hizi kutoka nchini Kenya.

Michezo ya hatua ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Alhamisi hii, kwa kuzikutanisha timu ya Dar Young African dhidi ya AFC Leopards wakati Nakuru All Stars ikikabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Gor Mahia zote hizi kutoka Kenya.
Michuano ya SportPesa Super Cup itaendelea tena kesho Michuano ya SportPesa Super Cup itaendelea tena kesho Reviewed by Zero Degree on 6/07/2017 03:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.