Loading...

Mtoto wa mwezi mmoja afariki dunia katika ajali ya moto mkoani Mwanza


Mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa mwezi mmoja aliefahamika kwa majina ya Faraja Simoni amefariki dunia kwa ajali ya moto katika kijiji cha Mbela wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa akiishi kwa mama mlezi Bi Eva Mnari miaka (37) mkazi wa kijiji cha mbela kutokana na mama yake mzazi kufariki ambapo imesemekana kuwa majira ya saa moja usiku mama mlezi alimlisha chakula kisha kumpeleka chumbani kulala na yeye akitoka nje kuendelea na shughuli nyingine wakati mama huyo akiwa nje anaendelea na shughuli zake aliona moto na moshi mwingi ukitokea chumbani alipolala marehemu ndipo aliita watu waje kumsaidia kuuzima moto huo.

Aidha imeelezwa kuwa wananchi wamefika na kufanya uokoaji kisha kutoa taarifa kituo cha polisi na askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kushirikiana na wananchi katika uokoaji, lakini tayari moto ulikua umeunguza godoro alilokuwa amelazwa marehemu na kumuunguza hali iliyosababisha marehemu kupoteza maisha papo hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mpaka sasa chanzo cha tukio hilo hakijafahamika.
Mtoto wa mwezi mmoja afariki dunia katika ajali ya moto mkoani Mwanza Mtoto wa mwezi mmoja afariki dunia katika ajali ya moto mkoani Mwanza Reviewed by Zero Degree on 6/21/2017 02:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.