Loading...

Mwakalebela naye aingia kwenye vita ya kuwania urais wa TFF


Fredrick Mwakalebela amechukua fomu za kuwania urais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Fredrick Mwakalebela baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais wa TFF
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Agosti 21 mjini Dodoma.

Mwakalebela alikuwa katibu mkuu wa TFF wakati wa uongozi wa Leodeger Tenga.

Baada ya hapo, aliamua kuachana na michezo na kuingia kwenye siasa akigombea jimbo la Iringa mjini kupitia CCM, hata hivyo alikatwa katika kura za maoni.

Alirejea tena katika siasa na kukutana na Peter Msigwa akiwa vizuri, akampiga chini.
Mwakalebela naye aingia kwenye vita ya kuwania urais wa TFF Mwakalebela naye aingia kwenye vita ya kuwania urais wa TFF Reviewed by Zero Degree on 6/18/2017 02:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.