Loading...

Orodha ya Vyuo Vikuu bora zaidi duniani kwa mwaka 2017


Orodha mpya ya kila mwaka ya vyuo vikuu bora zaidi duniani imetangazwa, ambapo chuo kikuu cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bado kinaongoza.

Vyuo vikuu vya Stanford na Harvard - pia kutoka Marekani - kadhalika vimeendelea kushikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.

Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1,000.

Vyuo vikuu hupimwa kwa mambo kama vile majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa.

Vyuo vikuu 10 bora zaidi duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings:
  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford
  3. Harvard
  4. California Institute of Technology (Caltech)
  5. Cambridge
  6. Oxford
  7. University College London
  8. Imperial College London
  9. Chicago
  10. ETH Zurich
Cambridge, Oxford, University College London na Imperial College London ndivyo vyuo vikuu pekee kutoka Uingereza ambavyo vimo kwenye kumi bora.

Kuna vyuo vikuu 76 vya Uingereza katika orodha hiyo ya vyuo vikuu bora, lakini waandalizi wa orodha hiyo wanasema vyuo 51 kati ya hivyo vimeshuka ukilinganisha na nafasi ya mwaka jana.

Vyuo Vikuu vya Uingereza vilivyo kwenye 200 bora orodha ya QS World University Rankings:

5. Cambridge
6. Oxford
7. University College London
8. Imperial College London
23. King's College London
23. Edinburgh
34. Manchester
35. London School of Economics and Political Science
44. Bristol
57. Warwick
65. Glasgow
78. Durham
82. Sheffield
84. Nottingham
84. Birmingham
92. St Andrews
101. Leeds
102. Southampton
127. Queen Mary, University of London
135. Lancaster
135. York
137. Cardiff
158. Aberdeen
158. Exeter
160. Bath
161. Newcastle
173. Liverpool
188. Reading

Inakadiriwa kwamba kwa jumla kuna vyuo vikuu kati ya 20,000 na 26,000 duniani 
kote.
Orodha ya Vyuo Vikuu bora zaidi duniani kwa mwaka 2017 Orodha ya Vyuo Vikuu bora zaidi duniani kwa mwaka 2017 Reviewed by Zero Degree on 6/09/2017 10:04:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.