Loading...

Rayvanny wa WCB ameshinda tuzo ya BET 2017


Hatimaye kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikiwa kunyakua tuzo ya BET. Tuzo hizo ambazo zimegaiwa usiku huu mjini Los Angeles, katika ukumbi wa Microsoft Theater Centre, Rayvanny ambaye alikuwa akiwania tuzo hizo kupitia kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act amefanikiwa kuibuka kidedea.


Wasanii wengine ambao alikuwa akishindana nao katika kipengele hicho ni Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica).

Baada ya kushinda tuzo hiyo, Ray kupitia mtandao wake wa Instagram ameshukuru kwa kuandika, “God is good all the time.Asante Mungu wangu Ulieniumba,Unaejua mwanzo na mwisho wangu.Uliyaona machozi yangu nilipokua mpweke sina furaha na mwenye majonzi mengi.WEWE NDIYE MUWEZA…”

“Asanteni wadau Wote mlio VOTE kwa Ajili yangu Ushindi umerudi Nyumbani.SITOACHA KUSHUKURU UONGOZI MZIMA #WCB @babutale @sallam_sk @Diamondplatnumz @mkubwafellatmk @kameboy_j @ricardomomo thanks Alot @bet_intl @betawards @bet_africa #WCBFORLIFE MAMA I LOVE YOU,” ameongeza.


Alichokiandika Diamond Platnumz baada ya Rayvanny kushinda tuzo ya BET 2017 kama ‘Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale
Rayvanny wa WCB ameshinda tuzo ya BET 2017 Rayvanny wa WCB ameshinda tuzo ya BET 2017 Reviewed by Zero Degree on 6/25/2017 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.