Shirika la Hifadhi za Taifa limetoa Tahadhari kwa wanaotembelea Hifadhi za Saadani
Meneja wa Mawasiliano wa Tanapa, Paschal Shelutete |
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka wakazi wa Dar es Salaam wanaotarajia kutembelea Hifadhi za Taifa za Saadani kutotumia njia ya Mkurunge Bagamoyo kwa kuwa miundombinu yake imeharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Meneja wa Mawasiliano wa Tanapa, Paschal Shelutete imeeleza kuwa miundombinu, ikiwamo madaraja na barabara vimeharibiwa na mvua.
“Hivyo basi wananchi na watanzania wanaotarajia kutembelea Hifadhi za Saadani wanashauriwa kupitia njia ya Msata-Mandera hadi Saadani na kwa wageni wanaotokea Tanga wanashauriwa kupitia njia ya Pangani-Mkwaja hadi Saadani,” imesema taarifa hiyo.
Shirika la Hifadhi za Taifa limetoa Tahadhari kwa wanaotembelea Hifadhi za Saadani
Reviewed by Zero Degree
on
6/01/2017 05:13:00 PM
Rating: