Loading...

Serikali imezindua mfumo mpya wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kielektroniki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akionesha Ipad maalumu aliyopewa ili kumuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwake ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuanzishwa kwa mfumo mpya wa serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kielektroniki, (Data Center) itakuwa dawa kwa wale wote wanaokwepa kulipa kodi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akishuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akizindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Akizindua uanzishwaji wa mfumo huo, jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema ili kuondoa malalamiko ya wale wanaodai kubambikiziwa kodi isiyo sawa na wale wanaokwepa kulipa kodi, ufumbuzi ni kuwepo kwa kituo hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akihutubia baada ya wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na na kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017
Amesisitiza kuwa ni lazima kila mmoja alipe kodi, ili kuweza kupata mapato yatakayoweza kutumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi.

Aidha ameyataka makampuni mbalimbali yaliyoko nchini, yakiwemo ya simu, na Wizara zote kuingia katika mfumo huo mpya wa serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya kielekroniki, ambao ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya nchi.

Rais Magufuli pia amesema kuanzisha kwa mfumo huo ni ukombozi wa kupunguza kero za muungano.

''...Kwa sababu ukijaza vocha yako huko Zanzibar hiyo pesa itaenza Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi hiyo pesa itakuja TRA Tanzania bara , hakuna mabishano, chombo hiki kinagawa chenyewe ndio faida yake...'' amesema Magufuli.

Serikali imesema imejenga kituo hicho kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa na taasisi za zake pamoja na makampuni binafsi yanayoendesha shughuli zao nchini.

Lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni dhamira ya serikali ya Tanzania katika kukuza na kuimarisha sekta ya Teknolojia na Habari na mawasiliano ambayo inakuwa kwa kasi ulimwenguni kote na ni kichocheo kikubwa cha uchumi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Bw. Joseph Kichere wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Serikali imezindua mfumo mpya wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kielektroniki Serikali imezindua mfumo mpya wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kielektroniki Reviewed by Zero Degree on 6/01/2017 04:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.