Loading...

Ugunduzi: Sayari nyingine 10 zenye uhai zagunduliwa


Wataalam wa maswala ya angani wametangaza ugunduzi wa sayari nyengine kumi angani ambazo huenda zinaweza kusaidia uhai.

Wanasayansi wa shirika linaloshughulikia maswala ya angani NASA wanasema kuwa data mpya iliochunguzwa kutoka kwa darubini ya Kepler inaonyesha sayari kumi zenye miamba ambazo zipo hatua chache kutoka kwa mkusanyiko wa nyota.

Sayari hizo ambazo zinatoshana na dunia, zote zipo nje ya jua katika mkusanyiko huo wa nyota.

Darubini hiyo ya Kepler sasa imegundua jumla ya sayari 50 katika maeneo tofauti yenye uhai angani.
Ugunduzi: Sayari nyingine 10 zenye uhai zagunduliwa Ugunduzi: Sayari nyingine 10 zenye uhai zagunduliwa Reviewed by Zero Degree on 6/20/2017 09:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.