Loading...

Abramovich amemfungulia Nemanja Matic milango ya kwenda Man United


Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Mmiliki wa Chelsea, Roma Abramovich ameingilia kati na kuruhusu Nemanja Matic auzwe kwa mashetani wekundu wa Uingereza.

Roman Abramovich amefungua milango kwa Nemanja Matic kujiunga na Manchester United lakini Chelsea wataongeza kile kinachoitwa ‘Ushuru wa Lukaku’ katika ada yoyote ya uhamisho.

Ripoti zinadai kuwa Matic ameelezwa kwamba matamanio yake ya kujiunga na United na kuungana kwa mara nyingine tena na kocha Jose Mourinho yatatimia kwa hiari ya klabu kwa kazi kubwa aliyoifanya pale.

Abramovich aliingilia kati pia ishu ya kuuzwa kwa Peter Cech katika mtindo huo huo na kumuacha aende zake Arsenal mwaka 2015 wakati Mourinho aliyekuwa meneja wa Chelsea kipindi kile, alikuwa kinyume kabisa na uhamisho huo.

Matic aliondolewa kutoka kwenye kikosi cha Chelsea cha kwenye michuano ya awali kabla ya msimu kuanza na siku ya alihamis 'Corriere dello Sport' walidai kwamba mazungumzo kati ya wakala wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 na mkurugenzi wa mpira wa miguu wa Juventus,  Fabio Paratici yalifanyika mwanzoni mwa wiki hii.

Ripoti hizo zinadai kwamba, Juventus hawako tayari kulipa ada ya paundi milioni 40 iliyotajwa na Chelsea, na kuiachia Manchester United.
Abramovich amemfungulia Nemanja Matic milango ya kwenda Man United Abramovich amemfungulia Nemanja Matic milango ya kwenda Man United Reviewed by Zero Degree on 7/22/2017 01:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.