Loading...

Serikali yawatangazia kiama majangili


SERIKALI imetoa onyo kwa watu wanaojihusisha na ujangili na kuwataka kuacha mara moja kazi hiyo na kutafuta shughuli nyingine, ikisema kamwe hawatakuwa salama.

Akitoa onyo hilo jana kwenye uzinduzi wa jengo la ukumbi wa kisasa wa maonesho uliopewa jina la Ziwa Nyasa uliojengwa na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kwa zaidi ya Sh bilioni tatu, Profesa Jumanne Maghembe (pichani) alisema mpaka sasa anawashikilia majangili wakubwa katika magereza mbalimbali nchini.

Alisema kazi ya ujangili sio salama kwa sasa, kwani serikali inapambana nao usiku na mchana kuhakikisha inatokomeza majangili wote, kwa usalama wa rasilimali za Taifa. “Nawashauri ingekuwa vizuri watu wanaofikiria kufanya ujangili bora watafute kazi nyingine maana haitakuwa na faida kwao na hawatabaki salama,” alisema.

Aidha alitumia fursa hiyo kuonya wafanyabiashara matapeli katika sekta ya utalii, ambao wanalaghai watalii kwa kuwasiliana nao katika mitandao kuwa wanawaandalia kila kitu na mwisho wa siku wanawaacha kwenye mataa.

Waziri huyo pia amempongeza Rais John Magufuli kwa kukazia mkazo wa kuondoa mifugo hifadhini, kwani ni kweli mtalii akifika hifadhini na kukutana na makundi makubwa ya ng’ombe haileti picha kwake na taswira ya nchi.
Serikali yawatangazia kiama majangili Serikali yawatangazia kiama majangili Reviewed by Zero Degree on 7/22/2017 01:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.