Loading...

AJALI: Wawili wafariki na wengine 36 kujeruhiwa baada ya daladala kugonga treni Jijini Dar


Watu wawili wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea leo asubuhi ikihusisha gari ya abiria aina ya coaster kukigonga kichwa cha treni maeneo ya Yombo Devis Kona.

Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamedai kuwa kuna majeruhi kadhaa ambao wamenza kufanya jitihada za kuwaokoa kutoka katika gari hilo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amesema watu wawili wamefariki dunia akiwamo mwanamke mmoja na mwanaume mmoja ambaye ni kondakta wa daladala hiyo.

Muroto amesema mbali na watu wawili kufariki pia kuna majeruhi 36 wanne kati yao wakiwa mahututi.

Amesema majeruhi mahututi ni wanawake watatu na mwanaume mmoja.

“Majeruhi wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na miongoni mwa majeruhi hao wanne wapo katika hali mbaya” amesema Kamanda Muroto.
AJALI: Wawili wafariki na wengine 36 kujeruhiwa baada ya daladala kugonga treni Jijini Dar AJALI: Wawili wafariki na wengine 36 kujeruhiwa baada ya daladala kugonga treni Jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 7/22/2017 12:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.