Loading...

Chelsea katika vita dhidi ya Real Madrid na Barcelona kusaka saini ya kinda huyu


Kwa mujibu wa ripoti, Chelsea sasa wameingia katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki, Malang Sarr.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 18 aling'ara vyema katika mchezo wake wa kwanza msimu uliopita.

Alifanikiwa kuifungia timu yake goli moja la ushindi dhidi ya 'Stade Rennais'. Beki huyo wa kati alifanikiwa kutokea uwanjani katika michezo 32 ambapo Nice ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligue 1 ya Ufaransa.

Na sasa, kwa mujibu wa taarifa ya 'Sky Sports', uwezo wake umemvutia meneja wa 'Stamford Bridge'. Taarifa inadai 'The Blues' wanamatamanio makubwa ya kumsajili kinda huyo.

Nice walimzawadia Sarr mkataba wake wa kwanza mnamo mwezi Novemba.

Mkataba huo bado umesalia na miaka minne ili kuisha lakini inasemekana kipengele cha kuuzwa kipo ndani ya dili hilo akikadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 36.

'Sky Sports' wanadai Chelsea watakutana na ushindani mkubwa kutoka kwa Barcelona na Real Madrid katika harakati za kusaka saini ya nyota huyo.
Chelsea katika vita dhidi ya Real Madrid na Barcelona kusaka saini ya kinda huyu Chelsea katika vita dhidi ya Real Madrid na Barcelona kusaka saini ya kinda huyu Reviewed by Zero Degree on 7/22/2017 01:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.