Loading...

Albamu mpya ya Jayz, 4:44 kinara kwenye chati za 'The Billboard 200'


Albamu ya 4:44 kutoka kwa rapper Jay Z inazidi kuendelea kufanya vizuri katika ulimwengu wa muziki kwa kuweza kushika namba moja katika chati za Billboard 200.


Kwa mujibu wa mtandao wa muziki wa Nielsen, albamu hiyo yenye nyimbo 10 na 14 kwa rapper huyo tangu aingie kwenye maisha ya muziki imekuwa moja ya albamu iliyo na uhitaji mkubwa zaidi kwa sasa.

Mpaka sasa 4:44 ndiyo albamu iliyoweka historia kwa miaka 61 katika chati za the Billboard 200 kuwa namba moja kwa muda mfupi.

Albamu hiyo imetaarishwa na producer No I.D. huku wasanii kama Beyoncé, Frank Ocean, Damian Marley, Kim Burrell, The-Dream wamesika pia kuna nyimbo kama vile ‘Bam’, ‘4:44’, ‘Marcy Me’, ‘Smile’, ‘Legacy’ na nyingine.
Albamu mpya ya Jayz, 4:44 kinara kwenye chati za 'The Billboard 200' Albamu mpya ya Jayz, 4:44 kinara kwenye chati za 'The Billboard 200' Reviewed by Zero Degree on 7/17/2017 12:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.