Loading...

Man United wameshinda vita nyingine dhidi ya Chelsea kwa kumnasa kinda huyu


Mashetani wekundu wamekamilisha usajili wa kinda mwenye umri wa miaka 16 kutoka Uholanzi, Millen Baars.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na mtandao wa 'Manchester Evening News', United wamefanikiwa kuipiku Chelsea katika vita ya kukamilisha usajili wa Millen Baars.

Man United hivi karibuni pia walifanikiwa kutibua dili la Lukaku aliyekuwa katika hatua nzuri kukamilisha uhamisho wake kwenda Chelsea na sasa wamefanikiwa kuitibulia Chelsea kwa mara nyingine 
tena.

Conte amekuwa akiripotiwa na mitandao mbalimbali kuwa mshabiki mkubwa wa kinda huyo na amekwisha tuma wanajeshi wake kumfuatilia kwa ukaribu zaidi. Hata baba yake mzazi pia, alithibitisha kuwa mwanaye huyo mwenye umri wa miaka 16 alikuwa akiwaniwa na Chelsea


Baars alikuwa ni mmoja wa vijana wa Academy ya Ajax, muonekano wake uwanjani na mfumo wa kikosi cha vijana cha Uholanzi vilimfanya avivutie vilabu vikubwa vya Uingereza. Alikuwa kwenye 'radar' za United wakati mwenzake, Kocha Louis Van Gaal alipokuwa meneja Old Trafford.
Man United wameshinda vita nyingine dhidi ya Chelsea kwa kumnasa kinda huyu Man United wameshinda vita nyingine dhidi ya Chelsea kwa kumnasa kinda huyu Reviewed by Zero Degree on 7/17/2017 12:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.