Loading...

Chadema yabisha hodi Takukuru kufuatia kujiuzulu kwa madiwani 7 wa chama hicho


Sakata la kujiuzulu kwa madiwani saba wa Chadema mkoani Arusha, limechukua sura mpya baada ya baraza la uongozi wa chama hicho mkoa, kuamua kulifikisha kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Gorugwa alisema hawaridhiki na mazingira ya baadhi ya madiwani kujivua nafasi zao za madaraka, ndiyo sababu ya msingi ya kulifikisha jambo hilo mbele ya vyombo hivyo ili vilichunguze undani wake.

Gorugwa alisema tayari wameandika barua ambazo watazikabidhi mbele ya vyombo hivyo.

Hata hivyo, Gorugwa alisema wanaotaka kuondoka Chadema wafanye hivyo mapema kwa kuwa safari yao bado ni ndefu.
Chadema yabisha hodi Takukuru kufuatia kujiuzulu kwa madiwani 7 wa chama hicho Chadema yabisha hodi Takukuru kufuatia kujiuzulu kwa madiwani 7 wa chama hicho Reviewed by Zero Degree on 7/15/2017 09:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.