Loading...

Chelsea wamekamilisha usajili wa mlinda mlango, Willy Caballero


Chelsea wamekamilisha usajili wa Willy Caballero kama ambavyo kwa upande wa Conte tayari amefanikiwa kumpata msaidizi wa Thibaut Courtois.

Caballero ameondoka Manchester City akiwa kama mchezaji huru na tayari rasmi sasa amesaini mkataba Stamford Bridge.

Atakuwa msaidizi wa Thibaut Courtois kufuatia Asmir Begovic kuelekea Bournemouth.


Caballero alisema: “Nina furaha kubwa sana kujiunga na Chelsea, Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.

“Ninatazamia kukutana na wenzangu na kuisaidia Klabu kupata mafanikio zaidi msimu ujao.”

Willy anakua mchezaji wa kwanza kwa kusajiliwa na Antonio Conte katika majira haya ya joto huku kukiwa na matarajio ya kuonekana kwa sura mpya nyingine
 nyingi pale Chelsea.

'The Blues' wako kwenye mazungumzo na beki raia wa Ujerumani Antonio Rudiger kutoka Roma.

Usajili wa Tiemoue Bakayoko na Alex Sandro nao pia uko mbioni kukamilika, kwa beki huyo wa kushoto kuweka record ya uhamisho wa ada ya paundi milioni 60.
Chelsea wamekamilisha usajili wa mlinda mlango, Willy Caballero Chelsea wamekamilisha usajili wa mlinda mlango, Willy Caballero Reviewed by Zero Degree on 7/02/2017 05:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.