Loading...

TFF imeahirisha uchaguzi mkuu hadi kamati kuu ya Utendaji itakapokutana


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza kuwa mchakato wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo umesimamishwa hadi Kamati ya Utendaji itakapokutana Juni 4, mwaka huu.

Tamko hilo limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumapili mchana kwenye ofisi za TFFzilizopo Karume jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi kukiuka taratibu.

Tayari zoezi la usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo urais lilikamilika jana Jumamosi tangu lilipoanza Alhamisi iliyopita huku wagombea wawili wakikosekana akiwemo Rais wa TFF, Jamal Malinziambaye anatetea nafasi yake ya urais na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ anayewania nafasi ya Makamu Rais wa TFF kutokana na wahusika hao kuwa rumande.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kudaiwa kufanya juhudi ili Malinzi afanyiwe usaili licha ya kuwa mahabusu wakati ambapo inaelezwa Kaburu aliandika barua ya kujiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi.
TFF imeahirisha uchaguzi mkuu hadi kamati kuu ya Utendaji itakapokutana TFF imeahirisha uchaguzi mkuu hadi kamati kuu ya Utendaji itakapokutana Reviewed by Zero Degree on 7/02/2017 05:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.