Loading...

Done Deal: Chelsea wamefikia makubaliano ya mwisho na Real Madrid kwa Alvaro Morata


Klabu za Chelsea na Real Madrid zimefikia makubaliano ya mwisho kuhusu ada ya uhamisho wa Alvaro Morata.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na 'Sky Italia'.



Ada yake ya uhamisho bado haijawekwa hadharani lakini ripoti zinatoa makisio tu, ambapo inadaiwa 'The Blues' wamelipa kiasi cha kuanzia paundi milioni 70 kukamilisha dili hilo la uhamisho wa nyota huyo kutoka Real Madrid.

Antonio Conte aliwahi kuhitaji kumsajili Morata kipindi yupo na Juventus mwaka 2014, hata hivyo, nyota huyo raia wa Spain aliwasili Juve wiki kadhaa tu baada ya Muitaliano huyo kuwa amejiuzulu kazi yake.

Pia, kwa mujibu wa 'Sky Italia', Alvaro Morata anatarajiwa kuondoka toka Real Madrid na kujiunga na Antonio Conte pamoja na Kikosi cha Chelsea nchini China.
Done Deal: Chelsea wamefikia makubaliano ya mwisho na Real Madrid kwa Alvaro Morata Done Deal: Chelsea wamefikia makubaliano ya mwisho na Real Madrid kwa Alvaro Morata Reviewed by Zero Degree on 7/19/2017 09:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.