Loading...

Mourinho anataka kumrithi Sir Alex Ferguson, ..asema yuko tayari kwa miaka mingine 15


Jose Mourinho anataka kuzifuata nyayo za Sir Alex Ferguson Manchester United na abakie kuwa meneja wa klabu kwa miaka 15.

David Moyes na Louis van Gaal hawakufanikiwa kukaa katika nafasi hiyo kwa kwa zaidi ya misimu miwili Old Traford, lakini Mourinho anaingia katika mwaka wake wa pili akiwa na Kombe la michuano ya EFL na lile la Ligi ya EUROPA mkononi ambalo pia lilifanikiwa kuipa kibali Manchester kushiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa (UEFA) kwa msimu ujao.

Mourinho hakufikisha zaidi ya misimu mitatu katika klabu zilizopita ikiwemo Real Madrid na Chelsea, lakini ameelekeza mipango yake ya kuleta mafanikio kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Ferguson.


"Niko tayari kwa hili," aliiambia ESPN. "Naweza sema niko tayari kwa miaka 15 ijayo." 

Mourinho aliiongoza United wakati ikipata mafanikio kwenye Ligi ya EUROPA na michuano ya EFL katika msimu wake wa kwanza kama meneja.

"Inanibidi niweke wazi jambo moja, kwamba ni vigumu sana kwa sababu ya mvutano uliopo kazini, kila mtu anamwandama meneja na wanachotazamia wao ni ushindi tu, lakini katika hali ya kawaida mshindi ni mmoja mchezoni na suala la kushinda linazidi kuwa gumu zaidi kadri miaka inavyozidi kusonga.

"Lakini, kitu ambacho nakifanya ni kuonyesha kwamba kazi yangu inaenda zaidi ya matokeo uwanjani, kwamba inaenda hadi kwenye maeneo ambayo watu hawatambui kama ni sehemu ya kazi ya meneja.


"Kwa nionavyo mimi, kazi yangu ni zaidi ya kile nikifanyacho uwanjani na matokeo ambayo timu yangu inapata wikendi.

"Katika klabu hii, jina la Sir Alex (Furgeson) ndilo pekee linalojulikana kwa miaka mingi sasa.

"Watu walizoea hivyo; watu waliyaelewa matokeo yaliyotokana na ubora wake. Baada ya David [Moyes] na Bw [Louis] Van Gaal, ninaelekea katika mwaka wangu wa pili na nina imani naweza kukaa hapa na kuipa klabu ubora inaouhitaji.

"Nitajaribu, lakini, nitajaribu pia kuwa na haki ya heshima hiyo na hicho ndicho huwa nakifanya kila siku niwapo kazini."


Van Gaal alitimuliwa kutoka kazini United baada ya kushinda Kikombe cha FA Cup Wembley, na Mourinho aliyetimuliwa Chelsea
 baada ya kubeba Kombe la Ligi Kuu anaamini kwamba atapata mafanikio mazuri msimu huu.


"Unapata mafanikio makubwa katika mwaka mmoja, mwaka unaokuja unakuwa hauna mafanikio kisha unafukuzwa," aliongezea.

"Ilinitokea nilipokuwa Chelsea, ilimtokea [Claudio] Ranieri Leicester, itawatokea wengine wengi zaidi. Siku hizi, watu wanamatazamio ya muda mfupi"
Mourinho anataka kumrithi Sir Alex Ferguson, ..asema yuko tayari kwa miaka mingine 15 Mourinho anataka kumrithi Sir Alex Ferguson, ..asema yuko tayari kwa miaka mingine 15 Reviewed by Zero Degree on 7/19/2017 10:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.