Loading...

Huyu ndiye mrithi wa nafasi ya Jerry Muro Yanga SC

Dissmas Ten (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari, Charles Boniface Mkwasa (kulia) akimsikiliza. Kushoto ni Godlisten Anderson ‘Chicharito’
Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa leo amemtambulisha Dissmas Ten kuwa Ofisa Habari mpya na wa nne wa klabu hiyo tangu mwaka 2010, akirithi nafasi ya Jerry Muro anayemaliza mkataba wake.

Louis Sendeu alikuwa Ofisa Habari wa kwanza wa Yanga mwaka 2010 chini ya Mwenyekiti, Wakili Imani Mahugila Madega aliyedumu hadi uongozi wa Mwenyekiti Wakili Lloyd Baharagu Nchunga kisha kutolewa mara baada ya kuingia kwa uongozi mpya wa Mwenyekiti Yussuf Manji.

Ambapo kijiti cha nafasi hiyo kilichukuliwa na Baraka Kizuguto aliyekaimu kwa muda kisha kuchukuliwa na Muro, lakini kabla ya kumaliza muda wake ndipo akakutana na rungu la adhabu kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ kwa makosa ya kimaadili.

Adhabu ya Muro imemalizika huku mkataba wake na klabu hiyo ukiwa nao umefikia mwisho na hivyo nafasi yake ikichukuliwa na siku chache baada ya kumaliza adhabu yake, Muro anaondolewa kazini na nafasi yake ikichukuliwa na Dissmas Ten .
Huyu ndiye mrithi wa nafasi ya Jerry Muro Yanga SC Huyu ndiye mrithi wa nafasi ya Jerry Muro Yanga SC Reviewed by Zero Degree on 7/14/2017 07:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.