Loading...

Manchester City yakimilisha usajili wa Kyle Walker kutoka Tottenham


Manchester City wamekamilisha ununuzi wa beki wa kulia wa Tottenham na England Kyle Walker kwa kitita cha £45m.

Walker, ambaye amechezea taifa lake mechi 27 na amekuwa na Spurs kwa msiimu minane, ametia saini mkataba wa miaka mitano City.

Uhamisho wake, ambao unakuwa na jumla ya £50m ukiongeza kikolezo cha £5m, huenda ukamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi wa England kuwahi kuwepo.

"Nina furaha sana kujiunga na City na nasubiri sana kuanza kucheza," amesema Walker.

"Pep Guardiola ni miongoni mwa mameneja wanaoheshimiwa zaidi duniani."

Walker alijiunga na Spurs kutoka Sheffield United mwaka 2009 na amecheza mechi 183 Ligi ya Premia.

Akiwa na Manchester City atavaa jezi namba 2, na anatarajiwa kusafiri na City Jumatatu kwa ziara yao ya Marekani.
Manchester City yakimilisha usajili wa Kyle Walker kutoka Tottenham Manchester City yakimilisha usajili wa Kyle Walker kutoka Tottenham Reviewed by Zero Degree on 7/14/2017 07:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.