Loading...

Lissu kusota mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika


Wakili anayemtetea Tundu Lissu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za uchochezi tangu jana, Fatuma Karume, amesema wamepeleka maombi katika Mahakama Kuu, ya kuiomba mahakama hiyo iiamuru Jeshi la Polisi kumpeleka Lissu mahakamani.

Wakati akizungumza na wanahabari, Karume amesema wamefikia hatua hiyo baada ya Polisi kusema wataendelea kumuweka mahabusu Lissu, hadi upelelezi wa shitaka linalomkabili utakapokamilika, ndipo watampeleka mahakamani.

Hata hivyo, Fatuma amedai kuwa, shitaka la uchochezi aliloshitakiwa Lissu lina utata kisheria kwa sababu polisi hawajaweka wazi mlengwa wa uchochezi huo.

“Kosa la kuchochea walilomshitaki lina utata sana, kuchochea tunavyoelewa sisi kisheria ina maana polisi ionyeshe ni nani umemchochea na kafanya jambo gani la uhalifu, lakini jana hawajasema amemchochea nani na kufanya jambo gani la uhalifu, wamesema kosa la kuchochea kama mabano,” amesema. 

Ameongeza kuwa “Niliuliza Lissu mtapeleka mahakamani lini, nikajibiwa bado wanaendelea kufanya upelelezi, jamani ina maana nchi hii tunakamata kwanza halafu upelelezi unafanyika baade? sababu ninanvyojua unafanya upelelezi, unamkata mtu na kumpeleka mahakamani. Kwa hivyo kama polisi wanadhani wanaweza kumkamata mtu bila upelelezi kukamilika ili waendelee kumuweka sero milele hiyo haiwezekani.”

“Tumeamua kwamba tutalipeleka Jeshi la Polisi mahakamani, mahakama kuu nimepeleka documenti mahakama Kuu, kuiomba iamuru polisi imlete Tundu mahakamani jumatatu, ili kama ana kesi aendelee na kesi. Wamkabidhi mahakamani na si kumuweka kwenye sero ya polisi mpaka wao wakimaliza uchunguzi wao . Tunataka tujue moja, wamuachie au wampeleke mahakamani afunguliwe kesi,” amesema.
Lissu kusota mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika Lissu kusota mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika Reviewed by Zero Degree on 7/21/2017 06:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.