Loading...

Tanzania yatajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii Barani Afrika.


Tanzania imetajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii Barani Afrika kwa mujibu mtandao wa Safari Bookings.com ambao ndio mtandao mkubwa wa ukuzaji wa safari za Afrika.

Mtandao huo ulifanya tathmini ya zaidi ya wataalam 2 , 500 na wale walioshiriki katika safari hizo kabla ya kutangaza kuwa Tanzania ndio eneo bora la safari mwaka 2017.

Tathmini hizo ziliandikwa na watalii walio fanya safari pamoja na wataalam bingwa wa Afrika.

Mtandao huo unasema kuwa uchanganuzi huo pia ulibaini kwamba Tanzania ilipata umaarufu wake kutokana na idadi ya wanyama mbali mbali.

Watu maarufu katika miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakizuru taifa hilo wakitembelea maeneo tofauti ya vivutio vya utalii nchini Tanzania.

Watu hao ni mwanamuziki maarufu USHER RAYMOND, aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United na Real Madrid DAVID BECKHAM, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool MAMADOU SAKHO, mchezaji wa Everton, MORGAN SCHNEIDERLIN na nyota wa filamu kutoka Marekani WILL SMITH na HARRISON FORD.
Tanzania yatajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii Barani Afrika. Tanzania yatajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii Barani Afrika. Reviewed by Zero Degree on 7/21/2017 06:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.