Loading...

Mabasi 11 yafungiwa kufanya safari za mikoani mkoani Arusha.


Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limefanya ukaguzi wa kushitukiza kwa mabasi ya kusafirisha abiria kwenda mikoani wilayani na maeneo ya vijijini na kugundua makosa mengi kwenye magari hayo ambapo zaidi ya mabasi arobaini yametozwa faini huku mabasi kumi na moja yakifungiwa kusafirisha abiria baada ya kukutwa na makosa makubwa yanayohatarisha uhai wa wasafiri.

Katika ukaguzi huo maafisa wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani wamegundua makosa mengi yakiwemo kukosa mikanda ya abiria uchakavu wa maumbo ya magari na kati ya zaidi ya mabasi hamsini yaliyokaguliwa madereva watano wenye makosa sugu wamefikishwa mahakamani.

Wakizungumzia operesheni hiyo wafanyakazi wa mabasi na mawakala wamekuwa na maoni tofauti wakati wengine wakidai kutopatiwa muda wa kutosha kufanya marekebisho wengine wameunga mkono zoezi hlo huku abiria wakieleza walivyoathirika.
Mabasi 11 yafungiwa kufanya safari za mikoani mkoani Arusha. Mabasi 11 yafungiwa kufanya safari za mikoani mkoani Arusha. Reviewed by Zero Degree on 7/26/2017 08:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.