Loading...

TCU yasitisha udahili kwa Vyuo Vikuu 19 kwa mwaka 2017/18


Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imesitisha udahili kwa Vyuo Vikuu 19 katika mwaka wa masomo 2017/2018 baada ya kubaini vyuo hivyo kukabiliwa na mapungufu mbalimbali.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa (TCU) Prof. Eleutheri Mwageni kwa vyombo vya habari ambayo imeeleza kuwa kutokana na uhakiki wa ubora wa elimu unaotolewa katika vyuo vikuu nchini uliofanyika kwa vyuo vyote nchini katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka 2016 tume hiyo ilibaini mapungufu ambayo yamesababisha kusitishwa kwa udahili huo.

Vyuo vilivyofungiwa ni Eckenforde Tanga University, Jomo Kenyatta University, Arusha, Kenyatta University, Arusha, United African University of Tanzania, International Medical and Technological University (IMTU) , University of Bagamoyo, St. Francis University College of Health and Allied Sciences, Archibishop James University College, Archibishop Mihayo University College pamoja na Cardinal Rugambwa Memorial University College.


Vingine ni Kampala International University Dar es Salaam College, Marian University College, St. Johns University of Tanzania Msalato Centre, St. Johns University of Tanzania, Marks Centre, St. Joseph University College of Engineering and Technology, Teofilo Kisanji University, Teofilo Kisanji University Tabora Centre, Tumaini University, Mbeya Centre, pamoja na Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMC.

Prof. Mwageni amesema kuwa kutokana na mapungufu yaliyobainika katika vyuo hivyo jumla ya programu 75 katoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ambapo uamuzi huo hautawahusu wanafunzi wanaoendelea na masomo katika programu za vyuo husika.
TCU yasitisha udahili kwa Vyuo Vikuu 19 kwa mwaka 2017/18 TCU yasitisha udahili kwa Vyuo Vikuu 19 kwa mwaka 2017/18 Reviewed by Zero Degree on 7/26/2017 08:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.