Loading...

Video: Bayern Munich walivyoiduwaza Chelsea kwa kichapo cha goli 3-2


Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata alianza mechi yake ya kwanza kwa kutoa pasi iliosababisha bao katika mechi ambayo timu yake iliopoteza 3-2 dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya kirafiki mjini Singapore.

Mshambuliaji huyo wa Uhispania aliyejiunga kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 60 ulioweka rekodi ya klabu kutoka Real Madrid wiki iliopita aliingia katika kipindi cha pili.

Huku Chelsea ikiwa imefungwa bao 3-1, Alonso aliugusa mpira wa kona uliopigwa na Cesc Fabregas na kumuwezesha Michy Batshuayi kufunga.

Bao la Rafinha na mawili ya Thomas Muller yaliisaidia Bayern kuibuka washindi kabla ya Marcos Alonso kuifungia Chelsea.


Video: Bayern Munich walivyoiduwaza Chelsea kwa kichapo cha goli 3-2 Video: Bayern Munich walivyoiduwaza Chelsea kwa kichapo cha goli 3-2 Reviewed by Zero Degree on 7/26/2017 08:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.