Loading...

Mdee apinga kauli ya Rais Magufuli


Mbunge wa Kawe na mwenyekiti wa BAWACHA, Halima Mdee amepingana na kauli na msimamo wa Rais Dkt. John Magufuli kuhusu agizo la wanafunzi wanapopata mimba na kujifungua wasiruhusiwe kurudi shule kusoma.

Mdee ameupinga msimamo huo huku akimtaka rais afuate sheria na katiba ya nchi inayowaruhusu watoto hao warudi shule baada ya kujifungua.

"Watu wanabakwa kwa sababu serikali imeshindwa kuwalinda watu wake, wanafunzi wanasoma mbali hakuna mabweni halafu watoto wasirudi shule pasipokujua ni kwa njia gani tatizo hilo limepatikana". Amesema Mdee.

Kwa upande mwingine ameongeza jambo kuhusiana na mchango alioutoa bungeni mke wa rais wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete.

"Nashangaa hata aliyekuwa 'First Lady' Mama Salma Kikwete naye anasimama kukataa watoto waliopata mimba wasirejee shuleni, wakati kipindi mume wake alipokuwa madarakani (Mh Jakaya Kikwete) alikuwa anatekeleza sheria ya kuwarejesha watoto waliobeba mimba shuleni" aliongeza Mh. Halima Mdee.

Suala la wanafunzi wanaopata ujauzito kutoruhusiwa kuendelea na masomo , limeibua mjadala mzito sana baada ya Mh. Rais kusema katika awamu ya serikali yake ya tano hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kuendelea na masomo akipata ujauzito.
Mdee apinga kauli ya Rais Magufuli Mdee apinga kauli ya Rais Magufuli Reviewed by Zero Degree on 7/04/2017 10:03:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.