Loading...

Watu 700 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini Somalia


Watu zaidi 700 wamefariki kutoka na mlipuko wa kipindupindu nchini Somalia, kulingana na baraza la wakimbizi la Norway. Mlipuko huo unadaiwa kuwa miongoni mwa milipuko mibaya zaidi ya ugonjwa huo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.


Baraza hilo limesema Sudan Kusini pia imeripoti visa visivyo vya kawaida vya ugonjwa huo.

Watu wengi haswa watoto wamefariki kutokana na kipindupindu zaidi ya vita nchini Somalia.

Sudan Kusini imerekodi vifo 160 kutokana na ugonjwa huo, ambao huwa nadra katika msimu huu wa kiangazi.

Hakukuripotiwa kisa chochote cha kipindupindu katika msimu kama huu mwaka jana.

Baraza hilo la wakimbizi la Norway limesema vita ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika nchi hizo mbili vimeharibu sekta ya afya na mfumo ya maji safi na maji taka.

Katibu mkuu wa shirika hilo, Jan Egeland amesema kuna hitaji la dharura la kupata maji safi, huduma za afya na dawa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
Watu 700 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini Somalia Watu 700 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini Somalia Reviewed by Zero Degree on 7/04/2017 09:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.