Loading...

Mourinho achukizwa na taratibu za usajili Man United


Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amedaiwa kutofurahishwa na taratibu za usajili zinavyoendelea wa kipindi hiki cha majira ya kiangazi katika klabu yake.

Baada ya United kutwaa taji la michuano ya Europa ligi, meneja huyo alisema alimpa makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward orodha na wachezaji anaowahitaji kusajili.

Man United haijafanikiwa kusajili wachezaji ambao kocha huyu anawataka katika kujenga kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao.

Kuna uwezekano kukawa na maendeleo mengine wiki hii lakini mpaka sasa ni mchezaji mmoja mpya aliyesajili ambaye ni beki Victor Lindelof toka Benfica ya Ureno.


Mourinho anahitaji mshambuliaji mmoja atakayeziba pengo la Zlatan Ibrahimovic, pamoja na kiungo mkabaji.

Man United wamekuwa wakimuwania mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata ambae uhamisho wake bado haujulikani hatima yake.

Lakini pia timu hiyo inawahitaji viungo Eric Dier wa Tottenham na Nemanja Matic kuja kujenga safu bora ya kiungo cha chini .
Mourinho achukizwa na taratibu za usajili Man United Mourinho achukizwa na taratibu za usajili Man United Reviewed by Zero Degree on 7/05/2017 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.