Loading...

Dully awaasa vijana kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa madawa ya kulevya

Msanii Dully sykes
Dully Sykes amewachana wasanii wenzake kwamba kinachowafanya washindwe katika tasnia ya muziki ni kutojitambua pamoja na kutokuwa na heshima.

Dully ameeleza hayo kutokana na uwepo wake wa kipindi kirefu bila ya kupotea au kupoteza kiwango chake katika suala zima la uimbaji tofauti na wasanii wengine ambao walikuwa pamoja kipindi cha nyuma lakini kwa hivi sasa wamepotezwa na upepo.

"Mimi najitunza, najielewa kama msanii, najitambua kwa kutengeneza 'status' yangu vizuri lakini wasanii wengi hawajitambui, mimi najitambua kuwa ni nani", alisema Dully.

Kwa upande mwingine, Dully amewaasa vijana wa sasa wakubaliane na maisha wanayoishi ili waweze kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa dawa za kulevya ambapo kwa sasa imekuwa ni janga la kila mahali.
Dully awaasa vijana kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa madawa ya kulevya Dully awaasa vijana kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa madawa ya kulevya Reviewed by Zero Degree on 7/05/2017 08:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.