Shirika la Hali ya Hewa duniani kuuingiza Mlima Kilimanjaro kwenye Program ya nchi zenye barafu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dakta Agness Kijazi anasema hiyo ni hatua ya msingi itakayotoa fursa kwa wataalamu wa hali ya hewa kufanya tafiti mbalimbali ili kubaini chanzo cha kupungua kwa kasi kwa barafu ya mlima huo mrefu barani Afrika.
Akizungumza na wataalamu wa hali ya hewa kutoka nchi zilizopo kwenye mpango huo wa wmo wanaokutana jijini Arusha kujadili uwepo wa barafu kwenye nchi za ukanda wa Tropiki,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo anasema hiyo pia itakua fursa kwa wataalamu kufanya utafiti kwenye maeneo mengine yenye barafu nchini.
Nchi nyingine ya ukanda wa Afrika Mashariki inayotajwa kuwa na eneo lenye barafu ni nchi ya Kenya kupitia mlima Kenya.
Source: ITV
Shirika la Hali ya Hewa duniani kuuingiza Mlima Kilimanjaro kwenye Program ya nchi zenye barafu
Reviewed by Zero Degree
on
7/05/2017 08:49:00 AM
Rating: