Loading...

PICHA: Maelfu wajitokeza kumuaga mtoto aliyekuwa shabiki wa Sunderland


Shabiki Bradley Lowery wa Sunderland alipoteza maisha wakati akipambana dhidi ya ugonjwa wa kansa.

Ujumbe wa kumsifu Lowery uliwekwa kwenye mabango barabarani
Simanzi ilikuwa kubwa kwa mashabiki wa soka England na duniani kote.

Wakati wa safari yake ya mwisho mtoto huyo aliyekuwa ana umri wa miaka sita, mashabiki wengi walionyesha huzuni kubwa akiwemo mshambulizi mkongwe wa Sunderland, Jermain Defoe.

Jamaa za Bradley walivalia jezi za soka, kukumbuka upendo aliokuwa nao kwa mchezo huo.

Mamake Gemma aliambia waliohudhuria mazishi hayo: "Alikuwa na tabasamu kubwa na la kupendeza hivi kwamba lilikuwa lingeangaza chumba chochote kile. Ni shujaa mwenye ujasiri, ametuacha.

"Aligusa nyoyo za wengi - aliwatia moyo watu wengi. Mwana wetu mpendwa, ndugu - nyota ya kupendeza.

"Ingawa wakati uliokuwa nasi ulikuwa mfupi, ni lazima una kazi ya kufanya huko mbinguni na malaika kwani Mungu amekuchagua wewe.

"Kwa sasa, mtoto wangu kwaheri, Hadi tutakapoonana tena shujaa wetu huko juu mbinguni."

Hiyo ndiyo safari ya mwisho ya Bradley.





PICHA: Maelfu wajitokeza kumuaga mtoto aliyekuwa shabiki wa Sunderland PICHA: Maelfu wajitokeza kumuaga mtoto aliyekuwa shabiki wa Sunderland Reviewed by Zero Degree on 7/14/2017 08:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.