Watumishi 450 waliotuhumiwa kuwa na vyeti feki warudishwa kazini
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro |
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema kuwa watumishi hao 450 ni kati ya watumishi 1500 ambao walikata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya serikali ya kutaka watumishi wenye vyeti feki kuacha kazi na kusitishiwa mishahara yao.
Mwanzoni wa mwezi wa tano mwaka huu serikali ya Tanzania ilitangaza kuwafuta kazi zaidi ya watumishi 9,932 ambao walibainika kuwa na vyeti feki na baadaye zaidi ya watumishi 1500 walikata rufaa kupinga maamuzi hayo ya serikali kwa kusema hawana vyeti feki, hivyo zaidi ya watumishi 400 wamethibitika kweli kutokuwa na vyeti feki na sasa watarudi makazini na kuendelea na majukumu yao.
"Kati ya hao wengine walikuwa ni wale ambo wameolewa na kupata majina ya waume zao kwa hiyo baada ya kuolewa majina ya wanaume zao yakawa yanatofautiana na majina yao yaliyopo kwenye vyeti, kwa hiyo wakati ule vilikuwa vinaonekana vile vyeti kama si vyao na kwa bahati mbaya Watanzania wanapoolewa wanachukua majina mawili ya wanaume zao badala ya kuchukua jina moja. Lakini pia kulikuwa na wengine majina yao ya kidato cha nne na kidato cha sita yalikuwa tofauti" alisema Ndumbaro.
Mwanzoni wa mwezi wa tano mwaka huu serikali ya Tanzania ilitangaza kuwafuta kazi zaidi ya watumishi 9,932 ambao walibainika kuwa na vyeti feki na baadaye zaidi ya watumishi 1500 walikata rufaa kupinga maamuzi hayo ya serikali kwa kusema hawana vyeti feki, hivyo zaidi ya watumishi 400 wamethibitika kweli kutokuwa na vyeti feki na sasa watarudi makazini na kuendelea na majukumu yao.
Watumishi 450 waliotuhumiwa kuwa na vyeti feki warudishwa kazini
Reviewed by Zero Degree
on
7/14/2017 08:03:00 PM
Rating: