Loading...

Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 3 mkoani Kigoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya siku tatu mkoani Kigoma kuanzia kesho.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amesema pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara katika wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu na Kigoma mjini, Mh. Rais ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami kilomita 50 katika wilaya ya Kakonko na Kilomita hamsini 50 katika wilaya ya Kasulu pamoja na mradi wa maji mjini Kigoma.

Amesema ziara hiyo ambayo ni ya kwanza tangu achaguliwe mwaka 2015 itatumika kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeo.
Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 3 mkoani Kigoma Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 3 mkoani Kigoma Reviewed by Zero Degree on 7/20/2017 06:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.