Loading...

Mavunde aja na mbinu ya kukomesha lugha chafu hospitalini


Baada ya kukithiri kwa malalamiko ya wagonjwa katika hospiatli ya mkoa wa Dodoma ya kutolewa lugha chafu na wahudumu wa afya mbunge wa jimbo la Dodoma, Anthony Mavunde, ametoa msaada na kuzindua mfumo wa CCTV camera hospitali hapo.

Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, akizungumza wakati wa kuzindua mfumo huo, amesema malalamiko ya wagonjwa kwa wahudumu wa afya wa hospitali hiyo, yamekuwa ni ya muda mrefu.

Kutokana na Dodoma sasa kuwa makao makuu ya nchi na kutegemea kupokea wageni wengi, msaada wa mfumo wa kamera katika hospitali hiyo utasaidia wauguzi na madaktari kufanya kazi zao kwa ufanisi kwa kuwahudumia wagonjwa kwa wakati ili kuondoa malalamiko kama hayo.

"Kupitia mfumo huu yale malalamiko ya muda mrefu yaliyokuwa yanalalamikiwa na wakati mwingine inawezekana ilikuwa ni uongo kwa sababu tumeshatengenezewa mentality tu kwamba tukienda hospitali tunajibiwa vibaya na kumbe ni katika uumbaji tu wa mwanadamu yupo mtu mmoja anaweza akafanya jambo wakachafuliwa watu wote. Lakini kwa sasa menejimenti itakuwa inaangalia rekodi ya lini tukio lilitokea na nani amefanya hivyo lakini hata muda pamoja na picha ya muhusika itaonekana " alisema Mh. Mavunde.

Mbali na msaada wa mashine hizo katika Hospitali hiyo, Mavunde pia ametoa msaada wa mashine ya biometrics kwa ajili ya lengo la kuwabaini wauguzi na madaktari ambao wamekuwa wakiondoka katika vituo vyao kabla ya muda na wale wanaofanya kazi muda wa ziada ili wapate stahiki zao.

"Wapo watu wanafanya kazi muda mrefu lakini ukienda kwenye vituo vyao hutapewa muda kamili utapewa muda tofauti lakini kupitia mfumo huu wa kisasa utaweza kuwasaidia kupata stahiki zao kutokana na kazi wanazozifanya. Mfumo huu unasaidia wagonjwa na watoa huduma" - aliongeza.
Mavunde aja na mbinu ya kukomesha lugha chafu hospitalini Mavunde aja na mbinu ya kukomesha lugha chafu hospitalini Reviewed by Zero Degree on 7/20/2017 06:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.