Loading...

Rais wa zamani wa Brazil, Lula da Silva ahukumiwa kifungo cha miaka 9 jela

Raisi wa zamani wa Brazili, Luiz Ignacio Lula da Silva
Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa unusu jela miongoni mwa kesi tano za ulaji rushwa zinazomkabili.

Lula aliondoka kutoka umaskini enzi za utoto wake na kuwa mmoja wa marais maarufu zaidi wa Brazil.

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha muungano alijizolea umaarufu kutoka jamii ya kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha Brazil.

Lakini sasa mambo yamegeuka na kukutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.

Hukumu hii inakuja wakati ambapo mtawala Lula akiwa ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani.

Kufuatia hukumu hiyo, rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wameapa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Wakati huo huo, kamati ya Bunge la Congress ya Brazil inajadili iwapo iiruhusu mahakama kuu kusikiliza kesi ya rushwa inayomhusisha Rais wa Brazil Michel Temer.

Temer alishtakiwa mwezi uliopita kwa tuhuma za kupokea hongo kutoka kampuni kubwa ya usindikaji nyama.

Kamati hiyo inatarajiwa kupiga kura hapo kesho.

Iwapo pendekezo hilo litapita, suala hilo litajadiliwa katika bunge dogo la wawakilishi, ambapo theluthi mbili itahitajika kupiga kura ili Rais ashitakiwe.
Rais wa zamani wa Brazil, Lula da Silva ahukumiwa kifungo cha miaka 9 jela Rais wa zamani wa Brazil, Lula da Silva ahukumiwa kifungo cha miaka 9 jela Reviewed by Zero Degree on 7/13/2017 08:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.