Loading...

Ujerumani yatwaa ubingwa wa mabara kwa mara ya kwanza


Mshambuliaji Lars Stindl ndie aliyeifungia Ujerumani goli pekee liliwapa ubingwa wa mabara kwa mara ya kwanza baada ya kutumia vyema makosa ya kiungo wa Chile, Marcelo Diaz.

Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Ureno walifanikiwa kutwaa medali ya shaba baada ya kuichapa Mexico kwa mabao 2-1.

Beki wa Ureno Luis Neto aliwapa Mexico goli la kuongoza baada ya kujifunga katika dakika ya 55, kabla ya Pepe kuzawazisha goli hilo katika dakika za lala salama.

Bao la mkwaju wa penati lilifungwa na Adrien Silva katika dakika ya 104 likawapa Ureno ushindi muhimu licha ya kumkosa nyota wake Cristiano Ronaldo.
Ujerumani yatwaa ubingwa wa mabara kwa mara ya kwanza Ujerumani yatwaa ubingwa wa mabara kwa mara ya kwanza Reviewed by Zero Degree on 7/03/2017 12:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.