Loading...

Wafanyabiashara wa mchanga waitapeli SMZ mamilioini


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetapeliwa mamilioini ya fedha baada ya baadhi ya wafanyabishara wa mchanga kuwasilisha risiti za malipo hewa zinazoonyesha fedha zimelipwa benki.

Akizungumza na wandisihi wa habari katika idara ya misitu ya Zanzibar Waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohamed amesema Wizara imegundua utapeli huo mkubwa ambapo baadhi ya wafanyabishara hao kwa kushirikiana na wafanyakazi wa benki ya Zanzibar wamekuwa wakipigiwa muhuri wa kuonyesha malipo yamefanyika na kufanikiwa kujipatia rasimali hiyo bila malipo.

Mhe Hamad Rashid anbaye ni Waziri kutoka Chama cha upinzani cha ADC ndani ya serikali ya Zanzibar amesema pia Wizara imegundua kuwepo udanganyifu ambao unaofanywa na wafanyakazi na wenye magari kubakika mchanga zaidi ya ule uliolipiwa na kusababisha ukosefu na upandaji wa bei ya rasilimali hiyo na tayari magari 49 yamekamatwa na Wizara inadai shlingi milioni 58 za faini huku mikakati mipya ikanza kuwekwa.

Hata hivyo baadhi ya watuhumiwa ambao walikuwa nje ya jengo la idara ya misitu wamekanusha kuwepo kwa udanganyifu huo wa kuchuja zaidi ya kiwango kilichukubaliwa na kudai wamekuwa wakilipa fedha za ziada ingawa Mwenyekiti wa jumuiya ya madereva na matajiri wa magari ya wauza mchanaga Msabaha Hassan Silima amekiri kuwepo kwa udanganyifu wa stakabadhi feki za benki.

Rasliamli ya mchnaga Zanzibar hivi sasa imekuwani malighafi hali kiswani Zanzibar ambapo gari la tani moja bei yake hufika hadi shlingi laki sita wakati serikali inauza kwa shilingi 27,000 huku serikali imelazimika kupiga marufuku uuzaji na biashara hiyo sasa inafanywa na serikali.
Wafanyabiashara wa mchanga waitapeli SMZ mamilioini  Wafanyabiashara wa mchanga waitapeli SMZ mamilioini Reviewed by Zero Degree on 7/06/2017 07:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.