Loading...

Walimu wanaotoa taarifa za wanafunzi wanaopata mimba shuleni watishiwa maisha


Serikali Mkoani Arusha imeliagiza Jeshi la Polisi Mkoani humo kushirikiana na wakuu wa shule za msingi na sekondari na kufuatilia kesi za wanafunzi wote waliopata mimba na taarifa zao kufikishwa kwenye vyombo vya dola bila wahusika kuchukuliwa hatua ili walioshiriki kuwalinda washughulikiwe ipasvyo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Bwana MRISHO GAMBO baada ya walimu wa shule za wilaya ya Arumeru kudai kuwa wanatishiwa maisha wanapotoa na kufuatilia taarifa za wanafunzi wanaopewa mimba na kukatishwa masomo.

Walimu hao wamesema wanafikia hatua ya kupata tamaa na kutoona sababu ya kuendelea kutoa taarifa za watoto wanaopata mimba kutokana na kuwepo kwa mtandao na vyombo vya dola wa kuwalinda wahusika.

Mmoja wa walimu wa shule hizo, Bwana HABIBU KABOGO amesema tatizo hilo limefikia hatua ya kutishia maisha ya wale wanaofuatila taarifa hizo kwa kuonekana kama wanafuatilia maisha ya watu na kibaya zaidi wamekuwa wakiishi karibu na wahusika.

Akitoa maelezo ya tuhuma hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Bwana CHARLES MKUMBO amekiri kuwepo kwa tatizo hilo alilodai kuwa linachangiwa zaidi na wazazi wanaoshirikiana na baadhi ya watendaji wasio waaminifu kupoteza ushahidi.
Walimu wanaotoa taarifa za wanafunzi wanaopata mimba shuleni watishiwa maisha Walimu wanaotoa taarifa za wanafunzi wanaopata mimba shuleni watishiwa maisha Reviewed by Zero Degree on 7/19/2017 09:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.