Loading...

Watu 8 wamefariki katika kisa cha kukanyagana nchini Senegal


Duru kutoka Senegal, zinasema kuwa watu wanane wameuwawa katika kisa cha kukanyagana, baada ya vurumai kutokea wakati wa mchuano wa mechi ya kandanda, kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Dakar.

Ukuta ulioporomoka ulikuwa umeunganishwa na viti vya kukalia uwanjani
Shirika rasmi la habari la serikali ya nchi hiyo- (APS), linasema kwamba mashabiki wa timu mbili za soka, walikabiliana baada ya mchuano wa soka uliochezewa katika uwanja wa michezo wa Demba Diop stadium, kumalizika.

Ukuta uliporomoka wakati ambapo idadi kubwa ya watu walikuwa wakiondoka kwa kasi uwanjani.


Idadi kubwa mno ya watu wamejeruhiwa katika Kisa hicho kilichotokea wakati wa fainali ya kuwania kombe la ligi kuu nchini humo, kati ya timu ya soka ya Stade de Mbour na Union Sportive Ouakam.

Mapigano yalianza kati ya mashabiki wa timu hizo mbili hasimu, hatua iliyowachochea maafisa wa polisi kuwarushia mabomu ya machozi. Hatua hiyo ilisababisha taharuki kubwa miongoni mwa mashabiki ambao walianza kukimbia na kusababisha mkanyangano, na kuporomoka kwa ukuta. Baadhi ya mashabiki walianza kurusha kila aina ya vifaa yakiwemo mawe.

Picha zinazosambazwa mitandaoni, zinaonesha watu wakikurupuka na kujaribu kupanda juu ya ukuta mfupi, huku wakizungukwa na wingu kubwa la moshi wa mabomu ya kutoa machozi.


Runinga ya taifa ya nchi hiyo, inasema kuwa, magari ya huduma za dharura na vikosi vya zima moto vilifika katika eneo la tukio hilo.
Watu 8 wamefariki katika kisa cha kukanyagana nchini Senegal Watu 8 wamefariki katika kisa cha kukanyagana nchini Senegal Reviewed by Zero Degree on 7/16/2017 10:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.