Loading...

Zanzibar imefutiwa uanachama wa CAF


Ikiwa imepita miezi minne tangu kukubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), shirikisho hilo limetengua uamuzi wa kuipa uanachama Zanzibar.


Rais wa CAF, Ahmad Ahmad amesema sababu ya Zanzibar kufutiwa uanachama ni kuwa sehemu ya Tanzania.

“CAF haiwezi kuzipa uanachama shirikisho mbili kutoka nchni moja,” alisema Ahmad na kuongeza.


“Maana ya nchi inatokana na nafasi yake kwenye Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN).”

Ikumbukwe kuwa Zanzibar ilikubaliwa kuwa mwanachama wa CAF kipindi Issa Hayatou akiwa Rais wa CAF.
Zanzibar imefutiwa uanachama wa CAF Zanzibar imefutiwa uanachama wa CAF Reviewed by Zero Degree on 7/21/2017 06:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.