Loading...

Chamberlain amekataa kusaini mkataba mpya Arsenal


Kwa mujibuwa wa taarifa ya 'SkySports', Chelsea na Liverpool wanatarajiwa kuingia kwenye mvutano mkubwa wa kumnasa Alex Oxlade-Chamberlain baada ya nyota huyo kukataa mkataba mpya alilopewa na Arsenal, mkataba ambao ungemfanya alipwe paundi milioni 180 kwa wiki.

Arsene Wenger alifanya mazungumzo na kiungo huyo raia wa Uingereza siku ya Alhamisi katika jaribio la mwisho la kujaribu kumbakisha Emirates.

Inaeleweka kwamba, Wenger atatoa uamuzi ndani ya masaa 24 yajayo iwapo atamruhusu aondoke Arsenal kabla ya dirisha la usajili kufungwa au atamwacha amalize mkataba wake na klabu ili aondoke kama mchezaji huru.


Oxlade-Chamberlain, ameshiriki katika michezo 27 na timu yake ya taifa, anaona mafanikio yake katika soka yako mahala pengine na 
ambapo muda huo huo, Chelsea na Liverpool wakiwa wamejiandaa kumnasa, wakitarajiwa kupeleka ofa ya zaidi ya paundi milioni 30 zilizotolewa awali na Chelsea mwanzoni mwa mwezi huu.

Nyota huyo aliyejiunga na Arsenal akitokea Southampton mwaka 2011, inasemekana hafurahii kucheza kama kiungo wa pembeni bali anapendelea kucheza katikati au kama kiungo mkabaji.

Wenger hatakuwa tayari kumuuza kwa maadui zake ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza, lakini klabu haitaweza kumwacha nyota huyo aondoke bure kama mchezaji huru, ilihali Mesut Ozil na Alexis Sanchez wakiwa katika mazingira kama hayo.
Chamberlain amekataa kusaini mkataba mpya Arsenal Chamberlain amekataa kusaini mkataba mpya Arsenal Reviewed by Zero Degree on 8/25/2017 05:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.