Loading...

Mwigulu atoa siku 7 wakimbizi kurudishwa nchini Burundi


Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ametoa siku saba kwa Shirika la Wakimbizi Duniani (Tanzania) kukamilisha taratibu za kuwarudisha Warundi walioomba kwa ridhaa yao kurudi nchini kwao Burundi.

Waziri Mwigulu amefikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa ya watu 8,743 ambao wamejisajili kwa hiari yao kurudi burundi wakiwa katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani kibondo mkoa kigoma, lakini wanakwamishwa na shirika la UNHCR ambalo wanasema wanataka kukaa vikao ndio waweze kiwarudisha.

Waziri Mwigulu amesema baada ya siku saba endapo UNHCR watashindwa kuwapeleka kundi la kwanza kwao basi yeye ataongea na waziri wa ulinzi kuomba kwa Amri jeshi mkuu Rais Magufuli magari ya kuwarudisha wakimbizi hao makwao.

Kwa upande wa mkuu wa makazi ya Nduta Peter Bulugu amesema kwasasa wanajumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 127,715 na kati ya hiyo watu 8,743 wameomba kurudishwa makwao na kuchelewa kurudishwa kuna pelekea sasa hali ya usalama kuwa si nzuri kwani kunawepo na vitendo vya vurugu za mara kwa mala kutoka kwa wakimbizi hao wanaotaka kuondoka.

Mkuu wa makazi amesema kupunguzwa kwa chakula kumechangia kuongezeka vitendo vya wizi ndani na nje ya kambi (wizi wa mifugo na mazao mashambani wizi wa taa za mitaani kambini (48 kati ya 217 zimeibbiwa) utekaji na ubakaji barabarani umeongezeka sasa.

Moja ya wakimbizi ambaye alikutwa anajiandikisha kurudi kwao amsema ameamua kujiandikisha baada ya kuambiwa kuna usalama kwao lakini pia changamoto wanazo kutana nazo za kupunguzwa kwa chakula walichokuwa wanapata mwanzo mpaka sasa kufikia kula mlo moja kwa siku ameona bora arudi kwend​a.
Mwigulu atoa siku 7 wakimbizi kurudishwa nchini Burundi Mwigulu atoa siku 7 wakimbizi kurudishwa nchini Burundi Reviewed by Zero Degree on 8/25/2017 05:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.