Loading...

Chelsea yapata ahueni kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham Jumapili


Habari za hivi karibuni kuhusu klabu ya Chelsea ni pamoja ya kuwepo kwa uwezekano wa kuongezeka kwa nguvu ndani ya kikosi ambapo inadaiwa kuwa, Eden Hazard na Timoue Bakayoko wako katika hali nzuri kiafya.

Kuna uwezekano mkubwa kwa Eden Hazard kurejea kuiongezea nguvu Chelsea katika mchezo wa jumapili dhidi ya Tottenham kwenye dimba la Wembley.

Hazard amekuwa nje ya dimba tangu alipopata majeraha kwenye kifundo cha mguu wakati timu yake ya taifa ilipokuwa kucheza ugenini mwanzoni mwa majira ya joto, hata hivyo alirejea dimbani kucheza dhidi ya QPR kwenye mchezo wa siri wa kirafiki uliochezwa jana Alhamisi ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa goli 8-0.

Hazard alionekana mwenye afya njema kimchezo na hata kufanikiwa kuifungia timu yake goli katika ushindi huo wa goli 8-0.

Tiemoue Bakayoko pia alijumuishwa kwenye mchezo huo, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana dimbani akiwa na uzi wa Chelsea tangu asaini mkataba wake akitokea Monaco.

Kiungo huyo amekuwa nje ya uwanja kufuatia kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti mwishoni mwa msimu uliopita.

Ripoti tayari zinadai kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwa wote wawili kucheza kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Chelsea na Tottenham HotSpurs jumapili kwenye uwanja wa Wembley.
Chelsea yapata ahueni kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham Jumapili Chelsea yapata ahueni kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham Jumapili Reviewed by Zero Degree on 8/19/2017 01:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.